Sunday, February 09, 2014

Mail on Sunday names and shames Kikwete and colleagues

UK based Mail on Sunday has published an article on how bigs shots in Tanzania government are corrupting a system that is bent on protecting endangered species, particularly our elephants. Click and read the story here: http://www.dailymail.co.uk/news/article-2554773/Tanzania-slaughters-11-000-elephants-year-bloody-trade-tusks-President-turns-blind-eye-Prince-really-shake-hands-him.html

Tuesday, March 12, 2013

Jihadhari na tapeli huyu anayetumia simu yangu

Kuna mtu ameibia simu yangu yenye laini mbili - Tigo (0719001001) na Airtel (0782172665) - tangu juzi, na anatumia namba hizo kutapeli pesa kwa watu ambao majina yao yamo kwenye contact list. Anawatumia watu meseji, hapigi wala hapokei simu anapopigiwa. 
Anadai kwamba mimi nina shida naomba msaada, na anapendekeza kiwango cha pesa za kutumiwa. Wapo wachache ambao wameibiwa tayari, na wengine walitaka kuthibitisha kama ni mimi, wakapiga simu hakupokea. 
Wanaojua namba zangu za simu wameniuliza kupitia simu yangu ya Voda, wakagundua ni mtego wa tapeli. Kwa taarifa hii, nawajulisha wote wanaonifahamu na wasionifahamu watakaoombwa pesa na mimi kutoka kwa yeyote, wasitoe kabisa. Anayeomba pesa hizo si mimi, ni tapeli!

Wednesday, March 06, 2013

Kibanda aumizwa kama Dk. Ulimboka

Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari, ambaye hadi Desemba 2012 alikuwa Mhariri Mtendaji wa Free Media, Absalom Kibanda, amevamiwa mbele ya lango la nyumba yake, Mbezi Beach, Dar es Salaam,  wakati anarejea kutoka kazini usiku; akapigwa; akang'olewa baadhi ya meno na kucha; akakatwa kidole na kuchomwa jicho. Kwa msaada wa watu mbalimbali, amesafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu. Tunafuatilia maendeleo ya matibabu yake.

Tuesday, February 26, 2013

Mdahalo wa pili urais Kenya 2013

Wasikilize wagombea urais wa Kenya katika mdahalo wa pili uliofanyika jana. Hawa hapa:

Sunday, February 10, 2013

Nukuu muhimu za leo katika mkutano wa Chadema, Temeke MwishoFreeman Mbowe:
“Tumegundua janja yao. Walidhani watauchakachua kila mara , tutatoka Bungeni; sasa tumeamua. Wasipotusikiliza hatutoki hadi kieleweke.”
“Wasio wana Chadema si adui zetu. Tuna jukumu la kuwashawishi, kuwabadili wawe wana Chadema, tuongeze idadi.”
“Watawala wanataka kutugawa katika makundi ya dini na ukabila ili watutawale kirahisi. Huu ni upumbavu, ujinga na ulimbukeni. Tusikubali kugawanyika.”
“Tuache kulalamika, tuchukue hatua.”

Dk. Willibrod Slaa:
“Bunge ni mahali patakatifu kuliko Ikulu.”
“Kamati ya Zitto haijavunjwa kikanuni; kwetu sisi haijaondolewa.”

Zitto Kabwe:
“Barabara ya Mtawara – Dar inajengwa kwa miaka minane (8) haijakamilika, lakini CCM na serikali yao wanasema wanataka kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar kwa miezi 18; na hawataki kutuinyesha mikataba.”
“Spika Anna Makinda hatumii akili yake. Anatumia akili za (William) Lukuvi na (Mizengo) Pinda.Lazima tumwajibishe kwa kumng’oa. Ama ang’olewe kwa nguvu ya umma au atumiwe meseji ajiondoe mwenyewe.”
ie nguvu ya umma kulazimisha utaratibu wa kupata katiba mpya. Haki isipotendeka tuingie barabarani, tuikomboe nchi yetu kwa miguu yetu na mikono yetu.”


Tundu Lissu:
“CCM na Makinda sasa waamue moja kati ya mambo haya mawili; ama waache Bunge lijadili hoja muhimu kwa taifa au Bunge lisiwepo kabisa.”
“TutumPeter Msigwa:
“Kinanaaa” Umma: “Weka mbali na tembo.”
“Nashangaa mimi si miongoni mwa wabunge wakorofi…nami nimo!”

Tuesday, January 29, 2013

Salaam na shukrani wa Wana Muleba


Ndugu zangu wapigakura wa Muleba,

Pokeeni pongezi za kipekee kwa kazi nzuri mliyofanya – kuleta ushindi mnono kwenu, kwa wanamageuzi nchi nzima na kwa chama chenu – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Ni ninyi, mabibi na mabwana, mlioleta ushindi katika uchaguzi wa vijiji na vitongoji uliopita ambamo mmevuna viti vya vijiji vitano na vitongoji 10.

Haya siyo matokeo yaliyonyesha tu kama mvua ya ghafla; ni matokeo ya mpango mkakati tuliouasisi – ninyi na mimi – hapo 29 Desemba 2012. Ni matunda ya mafunzo ya uongozi tuliyofanya katika kata zote 18 za jimbo tangu Februari 2012. Ni ushahidi kwa ujenzi wa misingi tuliyofanya pamoja katika maeno mbalimbali Muleba Kaskazini tangu Mei 2012; na Desemba 2012 Muleba Kusini.

Huu ni ushahidi mwanana wa kazi za wote ambao tulishirikiana kuandaa Kongamano Kuu la Jimbo na mikutano mikubwa ya hadhara tuliyofanya Septemba 2012 kwenye vituo vya Muhutwe, Kagoma, Kamachumu, Nyakatanga na Izigo. Bali hatukuwa peke yetu.

Makamanda wengi wameshiriki kikamilifu katika kuleta ushindi huu wa aina yake. Naomba kuwataja wachache, kwa niaba ya wengine wote waliokamilisha kazi hii. Kwa leo acha niwataje Salehe Mashaka, Symphorian Nkokerwa, Robert Rwegasira, Pontian Kaganda, Oliva Ishebabi, Medard Karwani, Zamda Salum, Emmanuel Mugalura, Joan Mary Rwegasira, Mzee Pangani, Ismail Bilyomumaisho, Leonigard Bayona na wengine wengi walioshiriki.  

Wapo pia makamanda kutoka nje ya Muleba ambao tulishirikiana kujenga chama hadi hatua hiyo. Wamo Godbless Lema, Alphonce Mawazo, John Heche, Kamanda Upendo, Concesta Rwamulaza, Peter Mweyunge, Renatus Kilongozi, Victor Sherejei, ambao, kwa nyakati tofauti, tuliwaalika jimboni kufanya kazi na waliitikia bila kusita. Ushindi huu ni wao pia kama ulivyo kwa wananchi wote wanaotafuta kukata minyororo ya utawala wa CCM.

Nakumbuka siku moja, ilikuwa Jumamosi, kabla ya kupiga kura, Karwani na Rwegasira mkaharibikiwa pikipiki mara nne mkitoka Ngenge na Bulyakashaju kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni. Poleni na hongereni!

Nakumbuka Ijumaa jana yake, katibu wetu wa kata Ngenge –anafahamika kwa jina la “Kakuru” –  alipigwa na kuuawa na watu wasiojulikana. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.

Katika mazingira ambamo CCM inanyang’anywa vijiji na vitongoji, hata kama ni kimoja; kwetu ni ushindi. Asitokee hata mtu mmoja kudai kwamba ni ushindi wake. Ni wetu sote. Hongereni makamanda. Leo hii, hatuhitaji kufanya utafiti mwingine. Hapana! Tayari tumejua kuwa ushindi utapatikana kwa maandalizi ya umma – ndani ya vyumba vyao; ndani ya nyumba zao, ndani ya vitongoji na mitaa yao; ndani ya vijiji, kata na wilaya zao. Hapa ndio kazi imeanza.

Aluta continua!  
My Photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'